News

Migos: Shilingi bilioni 9.46 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu

Published

on

Serikali imetangaza kwamba bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini HELB imesambaza shilingi bilioni 9.46 kwa wanafunzi 309,178 wa vyuo vikuu kote nchini.

Waziri wa Elimu nchini Julius Migos aliwahimiza wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuhakikisha wanafutilia fedha hizo kwa wavuti wa HELB kwani fedha hizo zilisambazwa kwa kila mwanafunzi aliyetuma maombi ya kupata ufadhili huo.

Waziri Migos alisema serikali imetimiza ahadi iliyotowa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ikiwemo kupunguzwa kwa karo ya vyuo vikuu, akisema serikali imejitolea kufanikisha elimu kwa wanafunzi nchini.

Aidha alidai kwamba kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 5.76 zitasimamia elimu ya ziada kwa wanafunzi wa vyuo vikuu huku shilingi bilioni 3.7 kuwasaidia wanafunzi kwa mahitaji mengine muhimu.

Usambazaji huo wa fedha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini umejiri kufuatia tangazo la serikali la ruzuku kwa HELB ya shilingi bilioni 5 ambazo zimechangia mgao wa HELB kuongezeka hadi shilingi bilioni 41 kutoka shilingi bilioni 36.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version