Sports
Milos Kerkez: Sasa Ni Mali Ya Liverpool
Kilabu ya Liverpool imetangaza kupata sahihi ya beki wa kushoto Milos Kerkez raia wa Hungary kutoka kilabu ya AFC Bounemouth ya Uingereza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amesajiliwa kwa pauni milioni 40 na tayari amemwaga wino kandarasi ya miaka mitano na The Reds.
Kerkez anakua sajili wa tatu kwa kocha Arne Slot ndaani ya liverpool msimu huu baada ya kuwasili kwa kiungo Florian Wirtz kutoka bayern Liverkusen sawa Jeremie Frimpong ikifikisha matumizi ya kilabu hiyo hadi pauni milioni 200 mpaka sasa msimu huu.
Raia huyo wa Hungary alijiunga na Bournemouth msimu wa mwaka 2023 akitokea AZ Alkmar na alikua nguzo muhimu akisaidia vijana hao kumaliza ndaani ya kumi bora.