News
Mkurugenzi wa huduma Center, Ben Kai aomboleza kifo cha babake
Mkurugenzi wa Huduma Centre Ben Kai Chilumo anaomboleza kifo cha babake Kuhani Lazaro Chilumo Kai.
Mzee Chilumo Kai alifariki Septemba 10, 2025 katika Hospitali ya Pandya mjini Mombasa, akiwa na umri wa miaka 94.
Mzee Chilumo atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kulihudumia Kanisa kwa zaidi ya miaka 60 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa makanisa mbali mbali miongoni mwayo ni lile la “The Light of God Evangelism” Tambarare lililoko Tezo mjini Kilifi.
Miongoni mwa waliojumuika katika kuomboleza na familia ya Ben Kai ni pamoja na Wakili George Kithi, aliyekuwa Seneta Christine Zawadi, Baha Nguma na Askofu Kombe Malo wa Kanisa la Tambarare.

Viongozi mbalimbali waomboleza kifo cha Kuhani Lazaro Chilumo Kai, wakiongozwa na Wakili George Kithi
Coco FM inaungana na familia ya Ben Kai Kuomboleza kifo cha mzee Kuhani Lazaro Chilumo Kai.
Bwana ametoa, Bwana amechukua, jina la Bwana lihimiziwe.
Taarifa ya Eric Ponda