News
Mnyazi: Eneo Bunge la Malindi lina Uhaba wa Maafisa wa Polisi
Mbunge wa Malindi Amina Mnyazi amesema idara ya usalama katika eneo bunge hilo inakumbwa na uhaba wa miundo msingi na ukosefu wa vifaa hitajika.
Mnyazi amehoji kwamba kwa sasa vituo vingi vya maafisa wa polisi eneo bunge la Malindi havina magari ya kutosha hali inayowalazimu wananchi kupitia ugumu kupata huduma za polisi.
Mnyazi amesema vituo hivyo vya polisi pia vinakumbwa na uhaba wa maafisa wa polisi licha ya wingi wa wananchi eneo hilo.
Hata hivyo amesema licha ya uchache wa maafisa hao wa polisi bado wengine wanapelekwa katika eneo la Shakahola, akilalamika kwamba eneo hilo pia halina mazingira mazuri ya kikazi.