Sports
Mshambulizi Wa Man.United Rashford Ni Mali Barca Ila Hataanza
Mshambulizi wa Manchester United Marcus Rashford akamilisha vipimo nchini Uhispania hapo jana.
Hata hivyo Baada ya Marcus Rashford kukamilisha vipimo hivyo vya afya kwa mafanikio huko Barcelona inaelezwa kuwa huenda asichezeshwe kwa mara ya kwanza kutokana na kutokuwa na utimamu wa kutosha wa mechi.
Rashford anatarajiwa kushiriki katika mazoezi yake ya kwanza akiwa na Barcelona hiyo hii leo ambapo mazoezi yake ya awali yataanza asubuhi na kuendelea hadi alasiri ili kumpa fursa ya kuhisi mazingira yake mapya.
Hafla rasmi ya kusaini mkataba imepangwa kufanyika kesho Julai 23 huko Spotify Camp Nou ambapo Rashford ataungana na Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta.
Mwingereza huyo pia atazungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza akiwa mchezaji wa Barcelona baada ya uwasilishaji wake.
Mara tu kila kitu kitakapokamilika, Rashford anatazamiwa kusafiri na Barcelona kwa ziara yao ijayo ya Asia.
Mechi yake ya kwanza kwa kilabu inaweza kuja wakati wa mechi za kirafiki ingawa usawa wake wa mechi ndio utakaoamua kama atacheza mara moja ambapo Klabu itatathmini hali yake mazoezini kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.
Chanzo: Mundo Deportivo