News

Mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya akamtwa Likoni, Mombasa

Published

on

Maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Inuka eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa wanamzuilia mwanamume mmoja baada ya kumkamata akiwa na misokoto 284 dawa za kulevya aina ya bangi iliyokuwa imefichwa ndani ya gunia.

Mshukiwa huyo, Bernard Odhiambo Ochieng’, alikamatwa na polisi eneo la Tongenyama baada ya kupewa taarifa na raia wema.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa polisi, Odhiambo alikuwa tayari amekamatwa awali na kuziliwa katika kituo cha polisi cha Ferry kwa makosa sawa na hayo ya ulanguzi wa dawa za kulevya, na aliachiliwa kwa dhamana wiki chache zilizopita.

Mamlaka ziliwahimiza wananchi kuendelea kutoa taarifa zitakazosaidia kukomesha biashara na matumizi ya dawa za kulevya katika jamii.

Uchunguzi zaidi unaendelea huku polisi wakiahidi kuendelea kushirikiana na wananchi ili kukomesha biashara haramu ya dawa za kulevya katika eneo hilo.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version