News
Mshukiwa wa wizi wa kimabavu akamatwa Likoni
Maafisa wa usalama eneo bunge la Likoni Kaunti ya Mombasa wanamzuiliwa mwaname mmoja kwa tuhuma za wizi wa kimabavu baada ya kuvamia hospitali ya kibinafsi akiwa amejihami na bunduki bandia.
Mwanamme huyo kwa jina Alfred Okoth mwenye umri wa miaka 27 alikamatwa baada ya kujaribu kuiba katika hospitali moja eneo la Konambaya huko Likoni.
Kulingana na polisi mwanamme huyo aliingia kwa siri katika hospitali hiyo na kuwatishia wafanyakazi pamoja na wagonjwa kwa kutumia bunduki bandia.
Maafisa wa polisi kutoka Kituo cha polisi cha Inuka waliingilia kati na kumwokoa mshukiwa kutoka mikononi mwa umati uliokuwa na ghadhabu, kabla ya kumpeleka kituoni kwa mahojiano zaidi.
Polisi walisema wanachunguza tukio hilo na kuwataka wananchi kuwa watulivu na kuepuka kujichukulia sheria mikononi mwao.
Taarifa ya Mwanahabari wetu