News
Mung’aro: Cancer Centre kukamilika hivi karibuni
Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro amesema sekta ya afya inatarajiwa kuimarika pakubwa kutokana na mikakati ya kuanzishwa kwa kituo cha kutoa matibabu ya Saratani yani Cancer Centre.
Akizungumza katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini, Gavana Mung’aro alisema kwamba katika kipindi cha miezi mitatu ijayo kituo hicho kitakuwa kimekamilika tayari kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Saratani.
Mung’aro alisema hatua hiyo itawaepushia wakaazi dhiki ya kwenda kaunti za nje ikiwemo Mombasa na Nairobi ili kusaka matibabu ya Saratani.
“Halafu huu mpango wa kuwachangia akina mama wetu na vijana, ningependekeza ufanyike kwenye kaunti ndogo zote za kaunti ya Kilifi”, alisema gavana Mung’aro
Aidha alikiri hatua hiyo itahakikisha usawa kwenye kuwayapiga jeki makundi hayo.
Kauli ya Mung’aro, ilijiri baada ya mpango huo wa kuwainua wanawake kiuchumi kufanyika katika eneo bunge la Malindi na Kilifi Kaskazini pekee siku ya Ijumaa 4 Julai 2025.
Taarifa ya Hamis Kombe