News
Mwanamume auwawa na Ndovu -Kavunzoni Ganze
Maafisa wa usalama kwa ushirikiano na wale Shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS, wamewatahadhari wananchi kuwa waangalifu dhidi ya Wanyamapori hasa Ndovu katika eneo la Ganze.
Hii ni baada ya Mwanaume mmoja kuuwawa na Ndoa, mchana wa Alhamis Agosti 14, 2025 katika maeneo ya Kavunzoni wadi ya Bamba eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi.
Kulingana na taarifa ya Polisi jamaa huyo aliyefahamika kwa jina la Stephen Rimba Gonja, anadaiwa kuwa mwalimu mstaafu wa shule ya msingi ya Kavunzoni alivamiwa na Ndovu akiwa shambani kwake na kutungwa pembe hadi akafariki.

Pembe ya Ndovu iliyovunjaka baada ya Ndovu kumuua mwanamume mmoja
Tayari maafisa wa KWS wameanzisha doria katika maeneo hayo kuhakikisha Ndovu wote walitangana na binadamu wanarudishwa mbugani.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi