News
Mwinyi: Magavana wameshindwa kuwajibika
Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amewakosoa magavana nchini, akisema wameshindwa kuwajibikia majukumu yao ipasavyo katika kaunti zao.
Mwinyi ambaye alikuwa akizungumza katika eneo la Portreiz eneo bunge la Changamwe, alisema Kongamano la Magavana ambalo lilifanyika wiki iliyopita lilionyesha wazi utepetevu miongoni wa magavana kinyume na matarajio ya Wakenya kwamba serikali za kaunti zingeimarisha maisha ya Wakenya hasa walioko mashinani.
Mwinyi alisema serikali za kaunti zimeshindwa kuwa na uwazi kuhusu namna zinavyopaswa kutumia fedha za umma pamoja na suala la ajira.
“Kila anayepewa nafasi anapaswa kufanya kitu cha kubadilisha ile sehemu’’, alisema Mwinyi.
Vilevile, Mwinyi aliwapongeza wabunge akisema wamepiga hatua katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo mashinani wakilinganishwa na Magavana.
Taarifa ya Janet Mumbi