News
Naibu Rais ahimiza utekelezwaji wa ugatuzi na Katiba nchini
Naibu Rais Prof Kithure Kindiki ameagiza maafisa wa serikali na wale wa kaunti kuja pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili mamlaka ya afya ya jamii nchini SHA pamoja na mikakati bora kutekelezwa.
Akizungumza alipoongoza kikao cha 28 cha baraza la bajeti na uchumi kati ya serikali kuu na zile za kaunti katika eneo la Karen jijini Nairobi, Kindiki alisema bima ya taifa Care inayosimamiwa na Mamalaka ya jamii nchini SHA ni kati ya mpango bora wa afya.
Kindiki alisema licha ya changamoto mbalimbali bado Ugatuzi umesalia kuwa suala muhimu katika Katiba, akisema serikali kuu na zile za kaunti ni lazima ziboreshe na kuuthamini ugatuzi na Katiba.
“Tuna jukumu la kuhakikisha afya inaboreshwa ndio maana ukiangalia bima ya taifa Care inayosimamiwa na Mamalaka ya jamii nchini SHA ni kati ya mpango bora wa afya, hivyo basi ugatuzi unafaa kutekelezwa kikamilifu
Naibu huyo wa Rais alisisitiza kwamba serikali hizo mbili ni lazima ziangazie madeni na kuyatatua mara moja kwani kufikia sasa madeni hayo ni zaidi ya shilingi bilioni 720.

Kikao cha 28 cha baraza la bajeti na uchumi kati ya serikali kuu na zile za kaunti katika eneo la Karen jijini Nairobi kilichowahusisha magavana na viongozi wa serikali kuu.
Wakati huo huo alitoa changamoto wa serikali za kaunti kufanya kazi na serikali kuu ili kutekeleza masuala muhimu ikiwemo kuboresh uchumi, kufanikisha miradi ya maendeleo, kubuni ajira, kuboresha sekta ya afya pamoja na elimu nchini.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi