Sports
Neymar Sehemu Muhimu Brazil
Mkufunzi wa Timu ya Taifa Brazil Carlo Ancelloti amemwambia mshambulizi wa kilabu hiyo Neymar ajiendae kwa kombe la dunia mwaka 2026
Kocha huyo aliyasema hayo muda mchache tu baada ya mchezaji huyo kuvunja mkataba na kilabu ya Santos ambayo amekua kwa mkopo kutoka AL-Hilal ya Saudia.
Kwa mujibu wa Ancelloti Neymar ni kiungo muhimu kwa timu yake na atamuhitaji kwa kipute cha Dunia mwaka ujao.
Neymar ndiye mfungaji bora kwenye kikosi cha Samba Boys na magoli 79.