News

Owen Baya akerwa na viongozi wa kaunti wasio na uadilifu katika utendakazi

Published

on

Mbunge wa Kilifi kaskazini Owen Baya amewataka viongozi wa kaunti ya Kilifi kujukumika katika utendakazi wao na kuangazia changamoto wanazopitia wakaazi.

Akizungumza katika kipindi cha Coco asubuhi, Baya alisema wakaazi wanahaki ya kupata hudumu bora baada ya viongozi kuchaguliwa na wananchi.

Kiongozi huyo alisema inasikitisha kuona wananchi wakiendelea kuhangaika hata baada ya kuchagua viongozi waliowaamini kwamba watatatua matatizo yao.

“Hii kaunti ya Kilifi tumekuwa hapa sasa tunaelekea miaka 15 ya ugatuzi, zile shida ambazo zilikuwa ugatuzi ulipoanza mpaka sasa ni zile zile, nikisema kwamba watu wanakunywa maji ya mtsara sisemi uongo, na inajulikana na watu wameona, swali ni, je tunafanya nini?”,aliuliza Baya.

Mbunge huyo sasa amewataka viongozi kutumia vyema pesa wanazopewa kutoka kwa serikali kuu kwa kuwanufaisha wananchi.

“Gavana huyo atapeana mwakilishi wadi milioni 45 kila mwaka wa kifedha, shilingi milioni za ufadhili wa masomo na shilini milioni 25 ustawishaji maendeleo katika wadi, wewe kama wadi yako watu wako na shida ya maji mbona usiitutue, unasubiri gavana aje akutatulie, na lazima tuambiane ukweli, mimi nataka niulize ni wadi gani hapa Kilifi haijapata takribani shilingi milioni 800 tangu serikali za kaunti zianze”,aliongeza Baya

Kuhusu suala la elimu Baya alishinikiza viongozi wenzake katika kaunti kuhakikisha wanalipa kipaumbele kwa kuboresha miundo msingi ya taasisi za elimu.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version