News

Owen: Uskwota umekithiri mno katika ukanda wa Pwani

Published

on

Mbunge wa Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi Owen Baya amesema kuwa uskwota umekithiri mno katika ukanda wa Pwani.

Katika mazungumzo ya kipekee na Meza yetu ya habari, Baya ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa alisema kwa miaka mingi pwani imekuwa ikikabiliwa na tatizo hilo hali ambayo imekuwa ikiwafanya wenyeji kuishi kwa hofu ya kufurushwa kutoka kwenye ardhi ambazo wanaishi.

Baya pia alisema kuna hazina ya makazi ambayo kila mwaka huwa inatengewa fedha ili kukabiliana na hali hiyo ya uskwota.

“Uskwota umekithiri kwasababu kwa miaka mingi watu walikuwa kidogo mwanzo, wakaanza kukaa mpaka wana wajukuu mpaka wana vitukuu wamekaa katika ardhi ambayo hawaimiliki’’ alisema Baya

Wakati huo huo, Baya alisema wanakabiliwa na changamoto kubwa katika ununuzi wa ardhi kutoka kwa wamiliki kwani baadhi ya ardhi zinakabiliwa na mizozo ya umiliki kati ya wanafamilia na mikakati inaendelezwa kuhakikisha tatizo la uskwota linapata suluhu la kudumu.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version