News
Polisi kutumia nguvu kukabiliana na wahalifu
Huenda maafisa wa polisi wakutumia nguvu kupita kiasi katika kukabiliana na wahalifu ama wale wanaolenga kuzua vurugu na fujo mashinani.
Idara ya usalama nchini imesisitiza kwamba itakabiliana kikamilifu na magenge ya kihalifu ambayo yanaendeleza uhalifu mashinani na kutatiza shughuli za kibiashara, uchumi na usalama wa taifa.
Idara hiyo ilisema tayari imebaini magenge ya kihalifu ambayo yanatatiza usalama wa wananchi, huku wazazi wakilaumiwa kwa kuwatetea watoto wao licha ya kufahamu kwa tabia hiyo inazidi kuhatarisha maisha ya jamii mashinani.
Idara hiyo, ililalamikia kukithiri kwa utovu wa usalama hasa kaunti za Kwale, Mombasa na Lamu katika ukanda wa Pwani, kutokana na vijana wengi kuzama katika uraibu wa Mihadarati na ukosefu wa kazi, hatua iliyopelekea baadhi ya vijana kujiunga na magenge ya mapanga.
Kauli hiyo ya idara ya usalama ilijiri siku moja tu baada ya Kamanda wa Polisi kanda ya Pwani Ali Nuno, kuagiza maafisa wa polisi kuwapiga risasi magenge ya kihalifu ya vipanga kwa kutatiza usalama.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi