News

Rais Ruto aingilia kati kuokoa mahusiano ya ODM na UDA

Published

on

Rais William Ruto ameingilia kati kuokoa uhusiano baina ya chama cha ODM na UDA wiki moja baada ya kamati kuu ya chama cha Odm kuzua tetesi, kuhusu matamshi ya baadhi ya viongozi wa UDA kwamba yanaenda kinyume na matarajio ya ushirikiano wao.

Rais Ruto na kinara wa chama cha ODM Oburu Oginga waliongoza mkutano huo wa maridhiano uliowaleta maafisa wakuu wa vyama hivyo viwili.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo ilisema mkutano huo ulijadili namna ya kuimarisha uhusiano wao huku pande zote zikikubaliana kuwapa wenyekiti wa vyama majukumu ya kuendeleza majadiliano.

Hii ni kwa lengo la kuweka msingi wa masuala muhimu yatakayohakikisha ushirikiano wao na usawa katika pande zote.

Rais Ruto na Oginga pia walikubaliana kubuni kamati ya usimamizi wa ushirikiano wao, utakao wajumuisha viongozi wa vyama mawaziri kadhaa na viongozi wa wengi na wachache bungeni.

Jukumu la kamati hiyo itakuwa ni kuhakikisha ajenda ya serikali inaendelea ipasavyo.

Pande zote zilikubaliana kufanya majadiliano, kuweka umoja na kuunga mkono mipango ya serikali.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version