News
Rais Ruto ameita saini mswada wa kukabili utakatishaji Fedha
Rais William Ruto ametia saini kuwa sheria mswada wa kupambana na utakatishaji Fedha na kufanyia marekebisho sheria ya kupambana na ufadhili wa ugaidi ya 2025.
Mswada huo, uliofadhiliwa na Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung’wah, ulilenga kuziba mianya ambayo imewezesha ufujaji wa pesa na mtiririko haramu wa kifedha, kupitia shughuli za kubadilishanaji raslimali.
Mswada huo ulifanyia marekebisho vipingee 10 vya sheria za bunge ili kukabiliana na mapungufu ya kiufundi ya uzingatiaji, yaliyobainishwa na kundi la kupambana na utakatishaji fedha haramu wa mashariki ya kusini mwa afrika (ESAAMLG).
Jopo la kifedha (FATF) linalojihusisha na harakati za kupambana na utakatishaji fedha haramu, kupambana na ufadhili wa ugaidi na kupambana na ufadhili wa kuenea pia yamehusishwa.
Rais Ruto na viongozi wa kiserikali wakati wa kutia saini mswada wa utakatishaji fedha
Sheria hizo zilizofanyiwa marekebisho ni pamoja na ile ya mapato ya uhalifu na kupambana na utakatishaji fedha haramu ibara ya 59 A, sheria ya kuzuia ugaidi ibara ya 59 B, na Sheria ya michezo ya kamari na bahati nasibu ibara ya 131, sheria ya mafao ya kustaafu sura ya 197.
Sheria nyengine ni ile ya madini sura ya 306, na sheria ya vyama vya ushirika ibara ya 490 B na sheria ya uhasibu ibara ya 531.
Taarifa ya Joseph Jira