News
Rais Ruto, amteua Claris Awour kuwa Mwenyekiti wa KNCHR
Rais William Ruto amefanya uteuzi mpya na kumteua Claris Awour Onganga kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu KNCHR.
Onganga anachukua nafasi hiyo baada ya Dkt Dancan Oburu Ojwang kukata wadhfa huo baada ya rais Ruto kufanya mabadiliko kadhaa katika taasisi mbalimbali za umma.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na Msemaji wa Ikulu ya Rais Hussein Mohammed, ilisema kwamba Rais Ruto pia amemteua John Cox Lorionokou kushikilia wadhfa wa Msajili mkuu wa vyama vya kisiasa nchini.
Agatha Wanjiku Wahome aliteuliwa kuwa Naibu msajili mkuu wa vyama vya kisiasa kufuatia mabadiliko aliyoyafanya rais katika taasisi mbalimbali za umma.
Hata hivyo majina ya walioteuliwa yatawasilishwa kwa bunge la kitaifa ambapo watu hao watapigwa msasa kabla ya kuidhinishwa rasmi na bunge ndipo waapishwa ili kutekeleza majukumu yao kisheria.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi