News
Rais Ruto kufungua rasmi kongamano la ugatuzi, Homabay
Kongamana la 9 la magavana nchini limeingia siku yake ya pili Agosti 13, 2025 katika kaunti ya Homabay ambapo masuala mbalimbali yanayohusu ugatuzi yanatarajiwa kujadiliwa na kuangaziwa kwa manufaa ya wananchi.
Rais William Ruto anatarajiwa kufungua rasmi kongamano hilo ambalo linaandaliwa katika shule ya upili ya wavulana ya Homabay huku viongozi mbalimbali kutokana mataifa ya kigeni pia wanahudhuria kongamano hilo katika kaunti ya Homabay.
Mwenyeji wa Kongamano hilo ambaye ni Gavana wa kaunti ya Homabay Gladys Wanga, alisema kwamba kongamano hilo linajumusha wakenya wote ambapo zaidi ya wajumbe elfu 30 wanahudhuria kongamano hilo katika kaunti ya Homabay.

Rais William Ruto pamoja na magavana wa kaunti mbalimbali {picha kwa hisani}
Gavana Wanga aliwahakikishia wajumbe wanaohudhuria Kongamano hilo kwamba usalama na mipango mingine imeimarishwa na masuala muhimu ya ugatuzi ataangaziwa katika kongamano hilo.
Gavana Wanga alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni ujumuishaji, usawa na haki ya jamii, ambapo Kongamano hilo litatamatika siku ya Ijumaa Agosti 15, 2025.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi