News
Ruto ahimiza umoja wa Afrika katika kutetea mageuzi
Rais William Ruto amewataka viongozi wa Afrika kuungana katika kupigia debe mageuzi ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Rais Ruto ambaye yuko mjini New York nchini Marekani kuhudhuria kikao cha themanini cha baraza kuu la umoja wa mataifa – UNGA, alisema kutengwa kwa Afrika katika baraza hilo hakukubaliki na hakuwezi kulindwa.
Kiongozi wa taifa aliongeza kuwa viongozi wa afrika lazima wapaze sauti ya Afrika katika kila kongamano, ikiwa ni pamoja na majukwaa ya nchi mbili, kikanda na kimataifa.
Alishinikiza umuhimu wa ushirikiano katika jitihada za uwakilishi wa haki katika baraza la usalama, katika kutetea msimamo wa pamoja wa afrika.
Wakati huo huo alidokeza kuwa afrika ina sehemu kubwa ya ajenda ya baraza la usalama na ni miongoni mwa wachangiaji wakubwa katika ulinzi wa amani wa umoja wa mataifa.
Taarifa ya Joseph Jira