Sports

Sare Ya Goli 1-1 Na Angola Mechi Ngumu Katika Taaluma Yangu Asema McCarthy

Published

on

Mkufunzi wa timu ya soka Harambee Stars ya Benni Mccarthy amesema kwamba mechi ya jana kati ya vijana wake na Angola ulikua ni mechi mgumu zaidi katika taaluma yake ya ukufunzi.

Kocha huyo aliyasema hayo licha ya kutoshana nguvu na Angola kwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Kundi A katika dimba la Moi Sports Centre, Nairobi.

Kwa mujibu wa McCarthy mechi hiyo haikua rahisi ila vijana wake walijituma asilimia mia moja kupigania nchi kwa mara nyingine mwalimu huyo akishukuru mashabiki lukuki waliofurika Kasarani kutazama vijana wa nyumbani.

Stars ilicheza mechi hiyo ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja baada ya kiungo Marvin Nabwire kuoneshwa kadi nyekundu mapema dakika ya 21 kipindi cha kwanza. Stars imejikusanyia pointi nne kwenye mechi mbili huku Angola ikiendelea kusubiri ushindi wake wa kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version