News
Sekta ya boda boda nchini kudhibitiwa na sheria kali
Sekta ya boda boda nchini sasa itakuwa inadhibitiwa na sheria kali, ikiwemo usajili mpya unaoonyesha maeneo maalum ya vituo pamoja na sare za rangi tofauti kulingana na maeneo wanayohudumu.
Hatua hizi zinalenga kukabiliana na ongezeko la visa vya uhalifu na uteketezaji wa magari ya watu binafsi na wanaboda boda.
Kulingana na kamanda wa Polisi jijini Nairobi George Seda kila kituo pia kitahitajika kuwa na mwenyekiti ambaye atawajibika na kukamatwa, tukio likitokea eneo hilo na likihusisha wanaboda boda.
Kulingana na kaununi mpya wahudumu hao watapewa usajili mpya kando na ule wa nambari za NTSA unaoonyesha wanapofanya kazi, kuanzia kaunti, kaunti ndogo hadi kituo cha abiria.
Taarifa ya Joseph Jira