News

Serikali inapanga kuajiri walimu wapya 2026

Published

on

Rais William Ruto amesema serikali yake imepiga hatua kubwa katika kuboresha viwango vya elimu nchini, huku ikijizatiti kuhakikisha kuna walimu wa kutosha katika taasisi zote za masomo.

Akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya jamii jijini Doha Qatar, rais Ruto alisema tangu utawala wake ulipochukua hatamu za uongozi miaka mitatu iliyopita, imefanikiwa kuwaajiri walimu 76,000, idadi ambayo inalenga kuongezaka hadi 100,000 kufikia Januari 2026.

Rais Ruto alidokeza kuwa hatua hiyo inalenga kutimiza pendekezo la shirika la umoja wa mataifa kuhusu Elimu (UNESCO) la kuwa na mwalimu mmoja kati ya kila wanafunzi 25 kufikia mwaka 2027.

Kiongozi wa taifa aaliongeza kuwa ili kuhakikisha wanafunzi wanapata soko tayari la ajira linalowiana na mahitaji ya kiviwanda na biashara, serikali yake imetekeleza jukumu muhimu la kupanua na kuongeza taasisi za kiufundi kote nchini

Taarifa ya Joseph Jira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version