News
Serikali ya kaunti ya Kilifi yashinikizwa kusimamia vyema miradi
Mkurugenzi mkuu wa shirika la World Vision Kenya Geophrey Kativa ameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kusimamia vyema miradi mbali mbali iliyotekelezwa katika eneo la Magarini baada ya kukamilisha kipindi cha miaka 18 cha kutoa huduma.
Kativa aliesema zaidi ya shilingi bilioni mbili zilitumika katika miradi ya elimu, kilimo na sekta nyengine muhimu.
Wakizungumza katika eneo la Marafa maafisa wa shirika hilo walisema kunaumuhimu wa miradi hiyo kutunzwa hasa miradi ya elimu ili kuendelea kunufaisha watoto wengi na kuinua viwango vya elimu katika eneo hilo.
Baadhi ya walionufaika na miradi hiyo kutoka shirika la World Vision wakiongozwa na Fridah Mganga walikiri kupokea elimu iliyobadili maisha yao, wakiitaka serikali ya kaunti ya Kilifi sawa na mashirika mengine kuendelea kuwainua wakulima ili waweze kujiendeleza kimaisha.
“Wakati World Vision ikiwa inatoka huku sehemu za Magarini, tunahitaji mashirika mengine na hata serikali ya kaunti itusaidie sisi wakulima hasa katika hii biashara ya mihogo ambayo tunaikatakata kutengeneza makopa, huwa tunahitaji vifaa kama driers, ambazo sisi hatuna”, alisema Fridah
Taarifa ya Joseph Jira