News

Serikali yaahidi kuboresha huduma za afya kupitia UHC.

Published

on

Waziri wa afya, Aden Duale, amesema serikali imeweka mikakati dhabiti kuhakikisha kila mkenya anapata huduma bora za afya kupitia mpango wa bima ya afya kwa wote (UHC).

Akizungumza wakati wa kufungua kongamano la 45 la kisayansi la chama cha wanafamasia (PSK), Duale alibainisha kuwa hatua hizo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za afya kwa zaidi ya asilimia 80, kuboresha mifumo ya utoaji huduma, na kuimarisha matumizi ya teknolojia ya kidijitali ili kuongeza uwazi, tija na thamani ya matumizi ya fedha katika sekta ya afya.

Waziri Duale aidha alieleza kuwa serikali inaendelea kukeleza mpango wa kuanzisha hazina ya bima ya afya kwa jamii (SHA) ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa nyuma, akisisitiza kwamba afya ni haki ya kikatiba na msingi wa maendeleo ya taifa.

Waziri Duale pia alitaja changamoto zinazokumba sekta ya mafunzo ya wataalamu wa afya, hasa kuibuka kwa taasisi za mafunzo ya famasia bila udhibiti madhubuti, hali aliyoitaja kuwa tishio kwa ubora wa elimu na huduma katika taaluma hiyo.

Kadhalika alibainisha kuwa utengenezaji wa dawa ndani ya nchi, kuboresha udhibiti kupitia bodi ya famasia na sumu (PPB), mfumo wa usambazaji wa dawa, kuimarisha usalama wa wagonjwa, na kujumuisha huduma za famasia katika mfumo wa bima ya afya ya kitaifa kuwa baadhi ya mambo yatakayopewa kipaumbele

Taarifa ya Mwanahabari wetu

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version