News

Serikali yabuni jopo la kuwateua viongozi wapya wa NCIC

Published

on

Waziri wa Usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, ametangaza kubuniwa jopo litakalomteua mwenyekiti na makamishna saba wa tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa (NCIC).

Kulingana na Murkomen, muda wa kuhudumu wa maafisa wa sasa wa tume hiyo inayoongozwa na Rev.Samuel Kobia, utakamilika Novemba 17, 2025, na kuhitimisha muhula wa miaka sita ulioanza Novemba 2019.

Jopo hilo la wanachama saba, litapewa jukumu la kuwatafuta wanaofaa kuchukua hatamu za uongozi kwenye tume hiyo.

Wanachama wa jopo hilo ni pamoja na Reuben Chirchir, Francis Meja, Pauline Mcharo, Alfred Mshimba, Michael Nzomo Mbithuka, na Jaji mstaafu Hannah Okwengu.

Tume ya NCIC imejukumiwa kuhakikisha mshikamano wa kitaifa, fursa sawa ya utangamano wa amani miongoni mwa wakenya wa tabaka mbali mbali na kidini.

Taarifa ya Joseph Jira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version