Business
Serikali yazindua mpango wa kuwasajili wakulima
Serikali imezindua mpango wa kuwasajili wakulima zaidi ya laki tano kupitia mfumo wa usimamizi wa kilimo.
Katibu katika idara ya Kilimo nchini Kiprono Runo alisema kuwa mpango huo ni muhimu katika kuafikia kanuni za bara ulaya zinazohitaji mashamba yote yaorodheshwe ili yaweze kuuza bidhaa zao kwenye masoko ya bara ulaya.
Kufikia sasa wakulima milioni 7 waliisajili kwenye mfumo huo tangu mwaka 2020, kwani serikali inalengo kuwasajili wakulima milioni 15 kufikia mwaka 2030.
Juhudi hizi zinalenga kuafikia mazao bora katika mashamba ya wakulima pamoja na kuhakikisha orodha ya wakulima nchini inabainika na serikali ili kuiwezesha kuwa na nafasi bora ya kuendeleza mipango ya ruzuku ya mbolea kwa wakulima nchini.
Shughuli ya usajili huo inafanyika katika kaunti zote 47 huku wakulima wakitarajiwa kujisajili kupitia afisi za kilimo kwenye kaunti.
Taarifa ya Pauline Mwango