News

SHA yasambaza shilingi bilioni 3.4 kwa hospitali nchini

Published

on

Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) inasema imetoa shilingi bilioni 3.4 kwa vituo vya afya kote nchini ili kulipa madeni chini ya Hazina ya Bima ya Afya ya Kijamii (SHIF).

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi 21, Agosti 2025, afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya SHA Mercy Mwangangi alisema fedha hizo zinagharamia huduma ya wagonjwa waliolazwa, matibabu ya waraibu wa dawa za kulevya, afya ya akili, huduma za wagonjwa mahututi na upasuaji.

Dkt Mwangangi alisema shilingi bilioni 1.09 za ziada zilitolewa kutoka kwa hazina ya huduma ya afya ya msingi, huku shilingi bilioni 1.7 nyingine zikishughulikiwa kwa ajili ya madeni ya huduma za matibabu ya kusafisha damu, saratani na upasuaji.

Kulingana na Mwangangi, Hospitali ya Nyandiwa Level 4 katika kaunti ya Homa Bay ilipokea shilingi milioni 19 kati ya mwezi Januari na Juni 2025 kwa wagonjwa wanaolazwa kwa muda mrefu pamoja na huduma za uzazi.

Alisema hospitali imethibitisha kupokea fedha hizo.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version