News

Sherehe za Chendachenda kuandiliwa Kwale mwaka huu

Published

on

Sherehe za kitamaduni za Chenda chenda za Makaya Tisa katika ukanda wea Pwani ambazo hufanyika kila mwaka, zimeratibiwa kufanyaika  katika kaunti ya Kwale mwaka huu.

Kikao cha Wazee kutoka Kaya zote za ukanda wa Pwani kimeamua kwa kauli moja kwamba sherehe hizo zifanyike kaunti ya Kwale ingawa haijaamuliwa ni wapi zitakakofanyika.

Sherehe hizo za Chenda chenda hufanyika Septemba Tarehe Tisa kila mwaka kwa malengo ya kuleta pamoja jamii za kimijikenda.

Kikao kilichotoa maamuzi hayo kilifanyika katika Kaya ya Ribe kaunti ya Kilifi kikiongozwa na Mshirikishi mkuu wa Makaya yote Mzee Boniface Tsuma aliyewahimiza wazee wote wa Kaya kuongea lugha moja ya kudumisha utamaduni wa wamijikenda.

Wazee wa Kaya wakitangaza Sherehe za Chendachenda kuandaliwa Kwale

Mwaka uliopita sherehe hizi zilifanyika eneo la Gotani gatuzi dogo la Kaloleni kaunti ya Kilifi ambako vurugu za kisiasa zilishughudiwa na kupoteza kabisa maudhui ya Sherehe hizo.

Taarifa ya Eric Ponda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version