News
Spika wa bunge la Kilifi Teddy Mwambire atemwa nje.
Bunge la kaunti ya kaunti ya Kilifi limepiga kura na kumtimua mamlakani Spika Teddy Mwambire.
Hii ni baada ya wawakilishi wadi 40 kati ya 51 kupiga kura ya kuunga mkono hoja ya kumtimua mamlakani Spika Mwambire iliyowasilishwa bungeni ya Mwakilishi wadi ya Tezo Thomas Chengo.
Naibu Spika wa bunge hilo Naftal Kombo alimuagiza karani wa bunge hilo Michael Ngala kuchapisha katika gazeti rasmi la serikali nafasi ya spika kuwa wazi.
Kombo alimtaka pia karani wa bunge hilo kutangaza wazi nafasi hiyo ili wakenya wenye tajiriba ya kujaza nafasi hiyo kuanzia kutuma maombi.
Hii inamaana kwamba spika Mwambire sasa sio spika tena wa bunge hilo na hatua hiyo huenda ikamueka nje ya mchakato wa kisiasa kwa kipindi cha miaka 10 kulingana na sheria na kanuni za katiba.
Spika Mwambire alitimulia kwa misingi ya ukiukaji wa katiba na sheria, kutumia vibaya ofisi ya umma pamoja na kuhujumu shughuli za bunge pamoja na kuwa mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi licha ya kushikilia nafasi ya umma.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi.