Sports
Tiketi za Stars Hazikuuzwa Zote
Rais wa FKF Hussein Mohamed amesema kwamba shirikisho hilo lilipata shilingi milioni 6.9 na wala si milioni 9.1 kama ilivyoripotiwa mechi ya Harambee stars dhidi ya Gabon Jumapili.
Kwenye hotuba kwa wanahabari Hussein ameweka wazi kwamba tiketi zote za mchuoano huo hazikuazwa (Sold out) kinyume na ilivyoripotiwa.
“Nataka niweke wazi kwamba kati ya tiketi 22,900 ambazo tulipewa na wahusika wa idadi ya mashabiki kuingia uwanja wa Nyayo ni tiketi 17,500 pekee ambazo ziliuzwa kwa mashabiki ila uwanja ulijaa hadi pomoni ,ukweli ni kwamba Kuna tiketi hazikuuzwa zote ukiwa na maana mashabiki wengine waliingia kinyume.
” Vyombo vya habari viliripoti kuuzwa kwa tiketi zote siku mbili kabla ya mchuoano huku pia shirikisho Hilo likithibitisha Hilo ila Rais huyo amekanusha kauli hiyo ya awali.