News

Tume ya EACC na Mamlaka ya IPOA zashirikiana kudhibiti ufisadi

Published

on

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC na Mamlaka huru ya kuchunguza utendakazi wa maafisa wa polisi nchini IPOA zimeahidi kushirikiana ili kupambana kikamilifu na ufisadi nchini.

Mwenyekiti wa Tume ya EACC Dkt David Oginde na Mwenyekiti wa IPOA Ahmed Isaack Hassan walisema taasisi zote mbili zinaendeleza mikakati ya pamoja ya kuimarisha uwajibikaji, ushiriki wa kijasusi na kusaidia mageuzi katika sekta ya usalama.

Dkt Oginde alisisitiza haja ya kuidhinishwa kwa mfumo wa kidijitali kwenye shughuli za polisi ili kupunguza sakata za ufisadi na kuingiliwa kwa binadamu, akisema utafiti wa kitaifa wa maadili na ufisadi wa mwaka 2024 ulionyesha kwamba polisi wanaongoza kwa ufisadi.

Maafisa wa Tume ya EACC wakiongozwa na Mwenyekiti Dkt David Oginde katika kikao cha kudhibiti ufisadi 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya IPOA, Ahmed Isaack Hassan alisema IPOA itafanyakazi kwa karibu mno na Tume ya EACC kupitia uchunguzi wa pamoja, mafunzo kuhusu maadili na uundaji wa programu za kupambana na ufisadi.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version