News

Tume ya huduma za polisi (NPSC) kuajiri maafisa wa polisi 10,000

Published

on

Tume ya kitaifa ya huduma za polisi (NPSC) imehakikishia wakenya kwamba zoezi lijalo la kuwaajiri maafisa wa polisi litakuwa wazi, shirikishi, na lisilo na utovu wa nidhamu.

Akiwa mbele ya kamati ya usalama ya bunge la kitaifa hapo jana Jumanne, afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Peter Leley alisema hatua zimewekwa ili kuhakikisha haki, ikiwa ni pamoja na matumizi ya waangalizi huru na zana za kidijitali.

Leley aliongeza kuwa uajiri huo pia utalenga jamii zilizo na uwakilishi mdogo na zilizotengwa kulingana na sera za kuchukua hatua.

Alisema tume hiyo imeshirikisha wadau wakuu, akiwemo katibu wa baraza la mawaziri wa mambo ya ndani, ambaye mchango wake umeingizwa katika mfumo wa ugawaji wa zoezi hilo.

NPSC inalenga kuajiri maafisa wa polisi 10,000 chini ya kanuni mpya iliyoundwa ili kukuza uwazi baada ya mazoezi ya hapo awali kugubikwa na malalamiko ya hongo na upendeleo.

Kati ya nafasi 10,000, nafasi 4,000 zimehifadhiwa kwa ajili ya vijana waliohitimu kutoka huduma ya kitaifa ya vijana (NYS).

Kwa mara ya kwanza, zoezi hilo litafanyika kupitia njia ya mtandao.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version