News

Tungule:Baadhi ya wenye timbo Jaribuni hawajaruhusiwa kuchimba madini

Published

on

Mbunge wa Ganze katika kaunti ya Kilifi Kenneth Kazungu Tungule amesema baadhi ya wawekezaji katika eneo la Jaribuni kaunti ya Kilifi wanaendelea kufungiwa timbo zahadi watakapokamilisha ahadi ya ujenzi wa barabara sehemu hiyo.

Akizungumza katika kipindi cha Coco Asubuhi Tungule alisema kwa sasa barabara inayoelekea kwenye timbo hizo imewekwa lami umbali wa kilomota 8 pekee, ikiwa imesalia kilomita moja.

Tungule aliesema ushirikiano baina ya wananchi na viongozi umefanikisha juhudi za kushinikiza wawekezaji sehemu hiyo kutekeleza ujenzi wa barabara sehemu hiyo.

“Lakini sasa waziri alipokuja viwanjani na akaona vile hali ilivyokuwa pia akakubaliana na sisi akasema nisawasawa hao wawekezaji ni lazima waweze kutengeneza hiyo barabara ndio maana tumefika pale tumefika, na bado kuna wengine ambao hawajafungua timbo zao tunatarajia pia hao wakitaka kurudia biashara zao wanafaa kuchukua kilimota moja yao”, alisema Tungule.

Awali wakaazi wa eneo la Jaribuni waliandamana na kufunga barabara inayoelekea katika timbo hizo wakilalamikia vumbi linalochangiwa na barabara mbovu.

Vile vile walidai afya ya wakaazi imezorota kutokana na vumbi linalochangiwa na malori ya kubeba madini sehemu hizo.

Ujenzi wa barabara ya Jaribuni kuelekea kwenye timbo za madini.

Hali hii ilichangia serikali kuu kupitia waziri wa madini na uchumi wa bahari Ali Hassan Joho pamoja na gavana wa kaunti ya Kilifi kuagiza timbo hizo kufungwa mara moja hadi wawekezaji watakapoweka lami barabara hizo.

Kuhusu matatizo yanayokumba wakaazi katika eneo bunge lake ikiwemo suala la uhaba wa maji, Tungule alisema ujio wa rais Kilifi umempa taswira kamili ya changamoto hizo akiamini kuwa rais William Ruto ataziangazia.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version