News

Ubalozi wa Kenya kuanzishwa jijini Vatican

Published

on

Baraza la mawaziri nchini limeidhinisha kuanzishwa kwa ubalozi wa Kenya katika jiji la Vatican hatua inayolenga kuboresha ushirikiano wa kidiplomasia na Vatican.

Taarifa ya baraza hilo iliyotolewa septemba 11,2025  inaeleza kuwa ubalozi wa kudumu katika Vatican utaongeza uhusiano wa pande mbili na kuendeleza ushirikiano katika amani, mabadiliko ya tabia nchi vile vile miradi ya kiutu.

Vatican ambayo ni makao makuu ya kanisa katoliki duniani inachukuliwa kama mhimili muhimu katika mazungumzo ya upatanishi na masuala ya kibinadamu.

Ubalozi huo pia unatarajiwa kuimarisha ushirikiano na mashirika ya kimaendeleo ya kikatoliki ambayo kwa sasa yanasimamia shule zaidi ya 7,700 na vituo vya afya 500 hapa nchini Kenya.

Baraza la mawaziri pia limeidhinisha kuanzishwa kwa ofisi nyingine za ubalozi huko Copenhagen nchini Denmark na Hanoi nchini Vietnam.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version