Sports
Uganda Yaponea Chupu Kuingia Robo Fainali Mashindano ya CHAN
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) yaliendelea kwa michezo yenye ushindani mkubwa ambapo Uganda na Afrika Kusini walitoka sare ya kufungana mabao 3-3 katika mchezo uliokuwa wa kusisimua mno.
Mchezo huo uliochezwa jana ulivutia mashabiki kutokana na kasi na mashambulizi ya pande zote mbili, huku kila timu ikionyesha dhamira ya kusaka ushindi. Uganda walitangulia mara mbili, lakini Afrika Kusini waliendelea kusawazisha hadi kufikia matokeo ya 3-3 kufikia mwisho wa dakika 90.
Katika mchezo mwingine, wenyeji Algeria walishindwa kutamba mbele ya Niger baada ya kutoka sare tasa ya 0-0. Licha ya kupewa nafasi kubwa kutokana na kuwa nyumbani, Algeria walikosa kutumia fursa walizopata, huku Niger wakicheza kwa nidhamu ya hali ya juu kuhakikisha wanabeba alama moja muhimu.
Kwa matokeo haya, Uganda Cranes sasa wamefuzu kwa robo fainali baada ya kumaliza kileleni na alama saba,Algeria imemaliza ya pili na alama sita huku Afrika kusini wakimaliza ya tatu na alama sita huku Niger na Guinea pia wakiaga mashindano hayo.