Business

Uhaba wa viwanda kaunti ya Kilifi wachangia ugumu wa uchumi

Published

on

Uhaba wa viwanda kaunti ya kilifi umetajwa kuchangia kudororan kwa uchumi.

Kulingana na wafanyibishara mjini Kilifi kaunti ya Kilifi, eneo hilo halina viwanda vya kutosha jambo ambalo linafanya biashara kuwa chini kwani wanategemea wakaazi pekee.

Wakizungumza na CocoFm, wafanyibiashara hao walisema uwepo wa viwanda katika kaunti unafanya idadi ya watu inaongezeka hivyo kufanya biashara kuimarika na uchumi kukua.

Waliitaka serikali kuu kwa ushirikiano na serikali ya kaunti kujenga na kufufua viwanda ambavyo vilifungwa ili kuinua uchumi na taifa.

“Wafanyibishara hapa Kilifi tunategemea wakaazi tu pekee yake kwani hatuna kampuni wala viwanda jambo ambalo linafanya biashara kuwa ngumu tena sawa, Ingekuwa bora kama serikali ingefungua viwanda na pia kufufua viwanda vilivyofungwa ili kusaidia biashara nyingi.”

Taarifa ya Pauline Mwango

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version