Business

Ukaguzi wa maonyesho ya Kilimo Mombasa unaendelea

Published

on

Kamati ya habari na mawasiliano bungeni ikiongozwa na mwenyekiti Wahome Wamatinga imefanya ziara yake katika uwanja wa maonyesho ya kilimo eneo la Nyali kaunti ya Mombasa.

Wamatinga ambaye pia ni Seneta wa Nyeri alisema ziara hiyo inalenga kutathmini maandalizi ya maonyesho ya kilimo ya mwaka huu ambayo yanatarajiwa kuanza tarehe 3 hadi 7 mwezi wa Septemba.

Wamatinga pia alisema wanapania kuweka kibanda maalumu ambacho kitatoa mafunzo ya utendaji kazi wa bunge kwa wale ambao watahudhuria maonyesho hayo.

“Tumekagua mahali ambapo tutakuwa tukijenga kibanda chetu na tumejadiliana yale mambo ambayo tutakuwa tukiyaonyesha’’ alisema Wamatinga.

Naye Mbunge wa Nyali Mohamed Ali alisema kibanda hicho kitatoa huduma zote za bunge kwa Wakenya ambao watahudhuria maonyesho hayo kauli ambayo iliungwa mkono na Mbunge wa Likoni Mishi Mboko ambaye aliwashinikiza wapwani kuhakikisha wanahudhuria maonyesho hayo.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version