News
Umoja wa upinzani waahidi kuungana licha ya pingamizi
Umoja wa upinzani umetangaza kwamba utaunga mkono mmoja wao ambaye atapambana na Rais William Ruto wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2027.
Viongozi wa Umoja wa upinzani ambao walihudhuria mkutano wa kitaifa wa wajumbe wa chama cha Peoples Liberation Party PLP, ulioongozwa na Kinara wake Martha Karua, viongozi hao wa upinzani wameapa kusalia pamoja.
Akizungumza baada ya Chama hicho cha PLP kumpa tiketi ya kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang’anyiro cha wadhfa wa urais wakati wa uchaguzi mkuu ujao, Karua alisema atambandua uongozi rais Ruto kuwa rais wa muhula mmoja.
Viongozi hao hata hivyo waliweka wazi msimamo wao wa kusalia pamoja na kumteua mmoja wao atakayepeperusha bendera ya umoja wa upinzani ili kumbandua rais Ruto mamlakani wakati wa uchaguzi mkuu mwaka wa 2027.

Viongozi wa umoja wa upinzani pamoja na wafuasi wa chama cha PLP wakati wa uzinduzi wa chama
Viongozi hao wa umoja wa upinzani ni pamoja na Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper, Martha Karua wa PLP, Rigathi Gachagua wa DCP, Eugine wa Wamalwa wa DAP-Kenya, na Justine Muturi wa Democratic Party.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi