News
Utafiti waonyesha magavana wachapa kazi
Utafiti uliyofanywa na kampuni ya Timely Kenya kuhusu uongozi na uwajibikaji wa serikali za kaunti umewaorodhesha baadhi ya magavana kama viongozi wachapa kazi.
Utafiti huo umemuorodhesha gavana wa Kwale Fatuma Achani kama gavana mchapa kazi nchini na aliyewajibika zaidi katika kipindi cha miaka mitatu tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Kulengana na utafiti huo, Gavana Achani amepata asilimia 56.6, akifuatwa kwa karibu mno na Gavana wa Murang’a Irungu Khangata akiwa na asilimia 56.4, nafasi ya tatu ikishikiliwa na Gladys Wanga wa Homabay kwa asilimia 54, Kimati Wamatangi wa Kiambu kwa asilimia 53.3, na nafasi ya tano ikishikiliwa na Gavana Ole Ntuntu wa Uasin Gushi kwa asilimia 52.8
Utafiti huo pia umeonyesha kwamba asilimia 61.8 ya wakaazi wa Kwale wanatambua majukumu ya viongozi wao na shinikizo lao limechangia viongozi kuwajibikia majukumu yao ya kikazi kwa kuambatana na kanuni na sheria za ugatuzi.
Wakati huo huo utafiti huo uliofanywa kati ya tarehe 3 na 11 mwezi huu wa Agosti, umeaggazia sekta za maji, afya, barabara na elimu, huku kaunti ya Pokot Magharibi ikiongoza na kufuatiliwa na kaunti ya Kwale, Kiambu, Narok na Homabay.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi