News
Utapia mlo unaikodolea macho Kenya
Kenya ni miongoni mwa mataifa manne barani afrika yaliyotajwa kuwa katika hatari ya kukosa chakula maalum cha kuokoa maisha ya watoto wenye utapiamlo katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Shirika la kimataifa la hisani kwa watoto, la Save the Children, lilisema hali hiyo itachangiwa na uhaba uliosababishwa na kupunguzwa kwa misaada.
Yvonne Arunga, mkurugenzi wa Save the Children katika eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika, alisema Agosti 28, 2025, wakati ambapo njaa inazidi kuutikisa ulimwengu, ufadhili ambao unaweza kuokoa maisha ya watoto umepunguzwa kwa sababu ya kukatwa kwa misaada hivi karibuni.
Kwa mujibu wa shirika hilo, ugavi wa vyakula maalum vyenye virutubisho na madini na huduma nyingine za kimatibabu, unapungua zaidi kwenye nchi za Nigeria, Kenya, Somalia na Sudan Kusini.
Taarifa ya Joseph Jira