News
Vijana waahidi kupigania mageuzi wanapojisajili kama wapiga kura wapya
Zoezi endelevu la kusajili wapiga kura wapya limeanza rasmi kote nchini huku idadi kubwa ya vijana wakijitokeza katika zoezi katika maeneo mbalimbali nchini.
Mjini Kilifi katika kaunti ya kilifi, vijana walijitokeza katika kituo cha usajili tawi la eneo bunge la Kilifi kaskazini, wengi wakisema wanataka kupigania mageuzi katika uongozi wa nchi hasa wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa 2027.
Vijana hao wamliambia Coco Fm kwamba wanataka kuleta mwamko mpya wa uongozi kwa kubadili viongozi ambao wameonekana kutojali maslahi ya mwananchi mpiga kura.
Walidai viongozi wengi walioko madarakani kwa sasa wameshindwa kutekeleza ahadi walizotoa kwa mpiga kura, wakishinikiza vijana wenzao kujitokeza kwa wingi kusajiliwa katika zoezi hilo.
“Matarajio yangu nikuwa tutapata viongozi bora, Kilifi tunahitaji viongozi wenye wataleta maendeleo pia ndio maana pia nimefanya maamuzi ya kuja kukata kadi ya kura”, alisema Purity Apiya mkaazi wa kilifi.

Baadhi ya vijana waliojitokeza kwenye zoezi la usajili wa wapiga kura mjini Kilifi.
Kwa upande wake Abdhul Mohammed Issa, Naibu msajili katika tume ya IEBC eneo bunge la Kilifi Kaskazini aliesema wanasajili watu ambao hawajasajiliwa kabisa pamoja na wale wanaotaka kubadili vituo vya kupigia kura.
“Tutakuwa tunaandikisha watu upya wale ambao hawajakata kabisa, wale ambao wanataka kubadilisha vituo vya vya kupigia kura, tuseme mtu anataka kuhama kituo chake tunamhamisha ama kama ni mtu anataka kuhama eneo lake la bunge pia tunamhamisha”, alisema Issa
Taarifa ya Joseph Jira