News

Vijana wahimizwa kutumia talanta zao kujiimarisha kiuchumi

Published

on

Vijana katika eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi wamehimizwa kutumia talanta zao kikamilifu ili kujikimu kimaisha.

Wakiongozwa na Samuel Mweni, vijana hao walisema kuwa idadi kubwa ya vijana eneo hilo na kaunti ya Kilifi kwa ujumla wana talanta mbalimbali ila wanakosa kutumia vipaji vyao kujiimarisha.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya vijana eneo la Rabai, Mweni aliwataka vijana kutoa kasumba ya kutaka kuajiriwa badala yake watumie talanta zao kujipatia kipato.

Kauli yake ilipigwa jeki na mlezi wa vipaji eneo la Rabai ambaye pia ni Mwanahabari Lolani Kalu ambaye alisisitiza haja ya vijana kuwa wabunifu na kutumia mitandao ili kujiuza akisema mtandao umerahisisha masuala mengi.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version