News

Viongozi wahimiza wakaazi kutouza ardhi zao kiholela

Published

on

Mwakilishi wa Kike kaunti ya Mombasa Zamzam Mohammed, amewataka wakaazi zaidi ya 400 waliopatiwa hatimiliki za ardhi katika eneo bunge la Jomvu kuzitumia vyema hati miliki hizo.

Akizungumza mjini Mombasa, Zamzam alisema wakaazi wengi wanapopata stakabadhi hizo muhimu huwa na hamaki ya kuuza mashamba yao, hali ambayo inawapelekea wengi wao kuishi maisha ya umaskini.

Aidha alisisitiza kwamba iwapo wakaazi watazitumia vyema hatimiliki hizo, watakuwa na uwezo kuchukua mikopo na kufanikisha miradi mbalimbali ya kuboresha maisha yao.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba, aliwahakikishia wakaazi wa eneo bunge lake kwamba hivi karibu watapata hatimiliki za ardhi huku akiwarai kutokubali kuhadaiwa na viongozi wa kisiasa kuhusu masuala tata ya ardhi.

Wakati huo huo Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharirf Nassir alisema Serikali ya kaunti hiyo imejitahidi kuhakikisha maeneo bunge yote yanafikiwa ili wakaazi awape hatimiliki za ardhi.

Hata hivyo, baadhi ya wakaazi walipewa hatimiliki hizo wamepongeza mpango huo wa serikali, wakisema zitasaidia pakubwa katika kujiendeleza kimaisha.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version