News

Viongozi wapendekeza Makanisa yote yasajiliwe

Published

on

Maafisa tawala eneo la Malindi kaunti ya Kilifi wametoa wito kwa wachungaji wa eneo hilo kuyasajili makanisa yao kwenye afisi za utawala mara moja.

Wakiongozwa na Chifu wa eneo hilo Wilfred Nyiro, maafisa hao tawala walisema kuwa kuna makanisa ambayo yamekuwa yakihudumu pasi na kusajiliwa.

Nyiro alisema kuwa hatua ya kutaka makanisa yasajiliwe ni njia mojawapo ya kukabiliana na ongezeko la wahubiri tata wanaohubiri itikadi potofu.

Chifu huyo pia alitoa wito kwa wakaazi kuwa makini katika kuwatofautisha wahubiri wa kweli na walaghai.

Haya yamejiri huku kaunti ndogo ya Malindi na Magarini ikitajwa kusheheni visa vya waumini kutapeliwa kwa misingi ya Imani.

Taarifa ya Hamis Kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version