Business
Viongozi Wataka Wafugaji Kilifi Wekeze Katika Uhifadhi wa Nyasi na Maji
Wafugaji kaunti ya Kilifi wameshauriwa kuhifadhi nyasi kwa wingi msimu huu wa mvua ili kuwawezesha kuwa na chakula cha kutosha kwa mifugo wao wakati wa ukame.
Kulingana na mjumbe maalum katika bunge la kaunti ya Kilifi Justin Rafiki, hatua hiyo itawapunguzia wafugaji wa ng’ombe changamoto za kutafuta lishe kwa mifugo wao wakati kiangazi.
Aidha Rafiki amewataka wafugaji kuwekeza zaidi katika uhifadhi wa maji na ununuzi wa dawa za mifugo ili kuimarisha kilimo cha ufugaji.
Kauli yake imeungwa mkono na mwakilishi wa wadi ya Kakuyuni Morris Hinzano na kuwataka wakulima kupanda nyasi za mifugo kwa wingi msimu huu wa mvua na kuzingatia uhifadhi wa maji kwa mifugo wao.