News
Visa vya Wasichana kudhulumiwa vyakithiri, Kilifi
Kaunti ya Kilifi imetajwa kuripoti visa vingi vya wasichana na wanawake kudhulumiwa kingono.
Haya ni kwa mujibu wa shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la International Justice Mission ambalo lilisema kwamba visa hivyo lilibainika kupitia takwimu.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Vincent Chahale alisema kuwa miongoni mwa dhulma hizo za kingono ni zile zinazotekelezwa na jamaa wa karibu wa wahasiriwa.
“Jamii inapaswa kuzamia suala hili ili kubaini chanzo chake kama njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa dhulma hizi zinadhibitiwa kikamilifu” alisema Chahale.
Chahale alihoji kuwa wanajamii wengi hunyamazia visa hivyo hasa wanapogundua kuwa watuhumiwa ni watu wao wa karibu hali inayopelekea wahanga wa visa hivyo kukosa haki.
Taarifa ya Hamis Kombe