News

Wadau wa mazingira wanaitaka sekta ya viwanda kuwajibikia taka za plastiki

Published

on

Wadau wa masuala ya mazingira katika kaunti ya Mombasa wanaitaka sekta ya viwanda kuwajibikia taka za plastiki wanazozalisha ili kuzuia uchafuzi wa Mazingira.

Wakiongozwa na Afisa wa Shirika la kimataifa la World Wide Fund for Nature, Henry Masai, wadau hao walisema wazalishaji wengi wanatumia plastiki kufungashia bidhaa zao lakini hawachukui hatua za kutupa plastiki hizo kwa njia salama.

Masai, alisema plastiki hizo huishia mitaani, baharini na maeneo ya wazi, hali ambayo inazidisha uharibifu wa mazingira na kuhatarisha afya ya binadamu pamoja na viumbe hai.

“Ni lazima sheria zizingatiwe katika masuala ya utunzaji wa mazingira kwani suala hilo limeathiri pakubwa afya ya binadamu, na viumbe hai hivyo basi sekta ya viwanda inafaa kuwajibikia taka za plastiki kikamilifu”, alisema Masai.

Wakati huo huo aliitaka idara ya usalama kuwachukulia hatua kali za kisheria wazalishaji wa plastiki wanaokiuka sheria za utunzaji wa mazingira, akisisitiza kwamba sheria zilizopo ni lazima zitekelezwe kikamilifu, akitoa wito kwa wananchi kutambua athari za taka za plastiki.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version