Business
Wafanyibiashara wa Shanga wavuna kutokana na watalii Mombasa
Wafanyibiashara kaunti ya Mombasa wanaendelea kuvuna zaidi kutokana na watalii wa ndani na nje waliozuru kaunti hiyo kufuatia maonyesho ya kimataifa ya Kilimo ambayo yalikamilika siku ya Jumapili.
Kulingana na wafanyibiashara wa kuuza shanga eneo la Lights kaunti ya Mombasa walisema idadi ya watalii ambao walitembelea eneo hilo imefanya biashara kuimarika.
Wakizungumza na CocoFm, walisema bei za Shanga zilipanda kutoka shilingi mia tatu hadi mia tano kwa shanga ndogo huku shanga kubwa zikiuzwa kwa shilingi elfu moja
Hata hivyo waliitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuimarisha usalama katika maeneo mengi ya kaunti hiyo ili kuwavutia watalii zaidi.
Taarifa ya Pauline Mwango