News

Wahadhiri chuo kikuu cha Pwani mjini Kilifi waendelea kugoma

Published

on

Shuguli za masomo zimeendelea kutatizika kwa siku ya saba sasa katika vyuo vikuu vya umma kote nchini kutokana na mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu uliaonza Jumanne Septemba 17, 2025.

Wahadhiri katika chuo kikuu cha Pwani mjini Kilifi kaunti ya Kilifi, wakiongozwa Rumba Mwachiramba walisema serikali siku ya ijumaa wiki jana ilitoa shilingi milioni 41 kwa chuo hicho japo pesa hizo hazijawafikia.

Mwachiramba alisema wataendelea kususia masomo hadi pale serikali itakapoafikia makubalioano yao.

Kwa upande wake naibu mwenyekiti wa muungano wa wafanyakazi katika chuo hicho UASU Violet Aura, alisema serikali inafaa kutekeleza matakwa yao matatu ya kuwalipa malimbikizi ya mishahara kama walivyokubaliana.

Mgomo huo umeendelea kutatiza shughuli za masomo huku wanafunzi hasa wale waliojiunga na chuo hicho wakishinikiza serikali kuelewana na wahadhiri ili waendelee na masomo.

Madarasa yamesalia bila wanafunzi katika chuo kikuu cha Pwani kufuatia mgomo wa Wahadhiri

Wahadhiri hao walitishia kuandaa maandamano makubwa jijini Nairobi Jumatano Septemba 24, 2025, katika juhudi za kuwasilisha ujumbe wao kwa serikali.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version